Kiungo Danny Drinkwater huenda akafungiwa michezo mitatu na chama cha soka nchini England (FA), kufutia tukio la kumpiga kiwiko Valon Behrami wakati wa mchezo wa ligi uliounguruma mwishoni mwa juma lililopita.

FA wanapewa nafasi kubwa ya kumuadhibu kiungo huyo kutoka nchini England, kufuatia kosa alilolifanya kutoonwa na muamuzi Neil Swarbrick aliyechezesha mchezo huo ambao ulimalizika kwa Watford kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Picha za televisheni zilimuonyesha Drinkwater akimpiga kiwiko Behrami na zinatarajiwa kutumika kama ushahidi katika vikao vya kamati ya nidhamu ya FA. Tukio hilo lilitokea katika dakika ya 67.

Kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kilijitokeza, baada ya dakika mbili kupita ambapo Drinkwater aliadhibiwa kwa kuonyeshwa kadi ya njano kwa kumfanyia faulo Brahimi.

Zinedine Zidane: Ronaldo Amefunga Mjadala Wa Ballon d'Or
Kagera watakiwa kutobweteke na misaada ya tetemeko