Meneja wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid Zinedine Zidane, ametuma salamu kwa wanaompinga Cristiano Ronaldo kuelekea kwenye kilele cha utoaji wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mwaka 2016 (Ballon d’Or).

Zidane ametuma salamu hizo, kufuatia maangamizi aliyoyafanya katika uwanja wa Vicente Calderón mwishoni mwa juma lililopita ambapo kikosi chake kiliongozwa na Ronaldo kuibanjua Atletico Madrid mabao matatu kwa sifuri.

Amesema mabao ya ushindi yaliyofungwa na Ronaldo, yatakua yamemaliza minong’ono na ubishi wa nani anastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2016.

Gwiji huyo wa soka nchini Ufaransa amesisitiza kuwa, ipo haja kwa mjadala huo kufungwa rasmi, kutokana na mchezaji wake kuendelea kuonyesha ubora wa soka dhidi ya wapinzani wake wanaotajwa.

“Sikuwahi kuwa na shaka kuhusu kiwango cha Cristiano, ninafahamu uwezo wake na ndio maana alifanikisha ushindi wa mabao matatu dhidi ya wapinzani wetu wakubwa.” Amesema Zidane

“Tunapaswa kuendelea kufanya kweli kama tunavyofanya sasa. Hatujashinda chochote mpaka sasa. Na tunakabiliwa na mtihani mzito wa mapambano dhidi ya wapinzani wengine waliobaki.” Aliongeza Zidane.

Jose Mourinho Arudisha Majibu Kwa Michael Carrick
Danny Drinkwater Kufungiwa Michezo Mitatu