Kampuni ya DataVision International, ambayo ilishinda tuzo ya Kampuni bora zaidi katika utoaji wa huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) mwaka 2019 (East Africa Brand Leadership 2019), imeanzisha mafunzo ya ukusanyaji takwimu kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mkuu wa kitengo cha TEHAMA kampuni ya DataVision International, Dkt. Shaban Kiwanga amesema kuwa mafunzo hayo yanatoa nafasi ya kujifunza mfumo wa TEHAMA ambao unarahisisha ukusanji wa takwimu bila kutumia karatasi.

“Mfumo huu unakupa nafasi ya kutumia simu au tableti ambazo unapotumia kukusanya takwimu, na ukimaliza dodoso lako moja kwa moja unalikuta kwenye mtandao, kwa kutumia mfumo wa tehama uitwao TIKITI,” amesama Dkt. Kiwanga.

Aidha Dkt. Kiwanga amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya kuadhimisha siku ya takwimu duniani ambayo ni tarehe 20 Oktoba kila mwaka.

Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwapa vijana stadi zenye kuleta tija kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania.

Bofya hapa…….

IGP Sirro: Magaidi zaidi ya 300 walivamia Mtwara
Ligi Kuu Tanzania Bara: KMC FC yatangulia Mwanza