Washindi wa vyombo vya moto vya Bajaji na Pikipiki kupitia kampeni ya ‘M-Pesa imeitika’, wameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji yanayopelekea wengi wao kujipatia mitaji ya aina mbalimbali na kuweza kumudu maisha.

Washindi hao, wameyasema hayo wakati walipomtembelea Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe ambaye naye amewataka kujibidiiisha katika kazi ili kujiletea maendeleo na kuipongeza kampuni ya Simu ya Vodacom kwa kuwa ya kwanza kwenye kuleta mabadiliko yanayoigusa jamii moja kwa moja.

Akiongea kwa niaba ya washindi wenzao, Magdalena Magoma na Beata Madachi, wamesema “Tunaishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi yanayoziwezesha kampuni kama Vodacom kuweza kufanya kazi kwa faida nchini, jambo linalonufaisha vijana kama wao na Taifa kwa ujumla.”

Washindi wa boda boda kwenye promosheni ya Vodacom “M-Pesa Imeitika” wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

Awali, Gondwe alisema, “Vodacom imeweza kuwa ya kwanza kwa kufanya M-PESA, Vodacom imeweza kuwa ya kwanza M-PAWA, Vodacom imeweza kuwa ya kwanza M MAMA na M MAMA inasaidia kina mama kuweza kufika hospitalini haraka na wakapata huduma, ni jambo kubwa sana.”

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya Godwin Gondwe amesema kupitia ‘M-Pesa Imeitika’ na huduma nyingine za Vodacom, vijana wanafikiwa na kuweza kutengeneza ajira akitolea mfano wa bajaji na pikipiki zilizotolewa kwa Vijana hao ambao wamejipatia ajira.

Kampuni ya Vodacom inaendelea kuwa kinara kwa kuwa wa kwanza katika mapinduzi ya kidigitali na kuwa na huduma zenye ubora na kugusa maisha ya Watanzania.

Mahitaji ya kibinadamu yahitaji Dola Mil. 160
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 31, 2022