Diamond Platinumz ambaye hivi sasa jina lake halikosekani kwenye matukio mengi makubwa ya muziki barani Afrika ikiwemo tuzo kubwa na shows, amempa shukurani ya kipekee Ambwene ‘AY’ Yesaya.

Kupitia instagram, kama sehemu ya kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa, Diamond amemshukuru AY kwa kumshika mkono na kumvusha daraja kuelekea level za kimataifa.

Hivi ndivyo alivyoandika:

“Misingi na Daraja Imara la kimataifa ulio tujengea na unayozidi kutujengea ndio leo inatusaidia vijana wako nasi kuweza kupenyeza na kutangaza kazi zetu kimataifa…Pengine watu Hawajui kuwa wewe ndio Uliye niwezeshea kufanikisha Collabo langu na Davido, Kuni Unga na Godfather na vingi ambavyo naamini ndio Mwanzo wa safari yangu ya Kimataifa… Nakuheshim sana Brother, na daima nitahakikisha sikuangushi…Happy birthday Bro @Aytanzania @Aytanzania @Aytanzania

Jerry Slaa Autosa Udiwani, Ausaka Ubunge Wa Ukonga
Cannavaro: Wachezaji Tunaumia Kuliko Mashabiki Wa Soka La Bongo