Tamasha la Nandy (Nandy Festival) jana ilibarikiwa na sauti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan lilipofanyika jijini Dodoma.

Nandy aliwa-surprise mashabiki wake baada ya kupokea simu na kuweka sauti ya juu (loudspeaker), na kuwasikilizisha salamu za moja kwa moja kutoka kwa Mama.

Rais Samia aliwaambia wananchi hao kuwa anawapenda na angependa awe katika tamasha hilo usiku huo, lakini kutokana na majukumu yaliyokuwa yanamkabili ameshindwa kuhudhuria.

Salamu hizo ziliamsha shangwe kubwa wakati Nandy akizifikisha, pembeni yake kulikuwa na baadhi ya viongozi wa jiji la Dodoma pamoja na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.

Rais Samia aliahidi kuwaunga mkono wanawake kuendelea kufanya kazi zao na kutengeneza ajira zaidi, alipozungumza na Wanawake jijini Dodoma, Juni 8, 2021.

Nandy Festival iliyozinduliwa mkoani Kigoma inazunguka mikoa ya Tanzania kama lilivyokuwa ‘Tamasha la Fiesta’.

Hati ya ardhi kutolewa kwa siku moja maonyesho ya sabasaba
Rais Samia akamilisha siku 100 kwa kishindo, ‘vicheko na mishangao’