Beki kutoka nchini Mali Mamadou Doumbia ameahidi kupambana mazoezini ili kulishawishi Benchi la Ufundi la Young Africans linaloongozwa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi.

Doumbia ambaye alisajiliwa Young Africans mwezi Januari mwaka 2023 akitokea  Stade Meliane ya nchini kwao Mali, amekuwa na wakati mgumu wa kuingia katika kikosi cha kwanza cha Young Africans, kufuatia mabeki aliowakuta kuwa na viwango Zaidi yake.

Akizungumza mchezaji huyo anayemudu vyema nafasi ya beki wa kati ameeleza kuwa kitu ambacho kinamfanya asipate nafasi tangu ajiunge na timu hiyo ni kufanyia kazi mifumo ya kiuchezaji ambayo wachezaji wenzake tayari wameizoea.

Mchezaji huyo ameeleza kuwa pamoja na changamoto hizo lakini hajakata tamaa ataendelea kupambana kupigania nafasi ya kucheza na anaamini siku chache zijazo ataanza kuitumikia timu hiyo.

Amesema mbali na kuyafanyia kazi maelekezo ya benchi la ufundi lakini pia amekuwa akijifunza kutoka kwa wachezaji wenzake.

Tangu alipotua Young Africans Doumbia amecheza kwa dakika 45, huku akikabiliwa na upinzani m kubwa kutoka kwa Nahodha Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Bacca pamoja na Yannick Bangala ambaye wakati mwingine huchezeshwa kama kiungo.

Edna Lema: Nitaweka Rekodi Ligi Kuu wanaume
Nasreddine Nabi aihofia TP Mazembe