Nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, Vincent Enyeama ameomba kujindoa katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Tanzania.

Enyeama ambaye ni kipa namba moja na tegemeo la Super Eagles ameomba kuondolewa kwa madai ya kifamilia.

Ingawa amesema ana matatizo ya kifamilia, tayari kuna taarifa kuwa kipa huyo hajafurahishwa kutoitwa kwa wakongwe Mikel Obi na  Victor Moses wakato Kocha mpya, Sunday Oliseh alipotangaza kikosi chake.

Hata kihivyo kipa huyo anayekipiga Ufaransa ataungana na wenzake katika hoteli waliyoweka kambi lakini haweza kuja Tanzania.

Shirikisho la Soka Nigeria (NFF), wala Oliseh hakuna aliyethibitisha hilo.

Chadema Yatoa Tamko Rasmi Kuhusu Aliyosema Dk Slaa
Simba Yaanika Kikosi Cha 2015-16