Michezo ya mzunguko wa pili wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inaendelea leo katika viwanja vitatu tofauti, huku kila timu ikisaka ushindi na kuweza kusonga katika hatua inayofuata itakayochezwa mwakani Januari, 2016 na bingwa kuwakilisha nchi mwaka 2017 katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CC).

Leo katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, African Lyon watawakaribisha Ashanti United, mjini Tabora Polisi Tabora watacheza dhidi ya Rhino Rangers na uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Sabasaba FC watawakaribisha Burkinfaso FC.

Kesho Jumatano kutachezwa michezo miwili, Friends Rangers watawakaribisha KMC katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, huku katika uwanja wa Sheihk Amri Abeid jijini Arusha, Madini FC watacheza dhidi ya maafande wa JKT Oljoro.

Alhamisi michuani hiyo itaendelea kwa michezo mitatu, Panone FC watawakaribisha Kiluvya FC uwanja wa Ushirikia mjini Moshi, Lipuli FC watacheza dhidi ya Kurugenzi uwanja wa Wambi – Mafinga, huku Mbao FC wakiwakaribisha  Geita Gold kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Mbowe azungumzia Kasi ya Magufuli, adai Hawako Tayari Kupinga Tu
Mwesigwa Afungua Kozi Ya Grassroot