Chama cha soka nchini England FA, kimemkuta na hatia meneja wa klabu bingwa nchini humo Chelsea, Jose Mourinho baada ya kupitia utetezi aliouwasilisha.

FA, wamejiridhisha na maelezo yaliyotolewa na meneja huyo kutoka nchini Ureno, baada ya kumtaka afanye hivyo majuma mawili yaliyopita, kufuatia maneno makali aliyoyatoa mara baada ya mchezo wa ligi ya nchini Engalnd, ambapo mashabiki walishuhudia Chelsea wakichabangwa mabao matatu kwa moja dhidi ya Southampton.

Mourinho, alimlaumu wazi wazi muamuzi wa mchezo huo sambamba na wasaidizi wake, kwa kuwataja kama chanzo cha kikosi cha The Blues kufanya vibaya, huku akisistiza waliwabeba kwa makusudi Southampton.

Kutokana na hali hiyo FA, imetangaza kumfungia Mourinho mchezo mmoja pamoja na kumtozaa faini ya paund elfu 50.

Adhabu hiyo, itachukua nafasi yake, katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo Chelsea watakua wageni wa Aston Villa huko Stamford Bridge.

Hata hivyo Mourinho amepewa onyo kali la kuhakikisha harudii tena makossa hayo, kutokana na kubainika msimu huu imekua ni mara yake ya pili kuwatuhumu waamuzi mbele ya waandishi wa habari.

Kwa mara ya kwanza Mourinho alifanya hivyo mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Man City, ambapo kikosi chake kilikubali kulambwa mabao matatu kwa sifuri.

Luka Modric Kuikosa Levante
Kuhusu Kufungwa Rasmi Uchumi ‘Supermakets’ Tanzania, Uganda