Chama cha soka nchini England FA, kimemfungulia mashtaka mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Diego Costa, pamoja na beki wa Arsenal Gabriel Paulista.

Wawili hao wamefunguliwa mashataka na FA kutokana na kadhia iliyojitokea mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa ligi ya nchini Engalnd ambapo Chelsea walifanikiwa kuwafunga Arsenal mabao mawili kwa sifuri kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Wachezaji hao walionekana wakishikana na kukaribia kizichapa katika dakika ya 43 ya mchezo, baada ya Diego Costa kumfanyia vitendo visivyo na nidhamu beki Laurent Koscielny.

Costa alionekana akimpiga Koscielny usoni na kisha alimsukuma kwa kutumia kifua chake na Gabriel alipojaribu kumuuliza mshambuliaji huyo kwa nini alifanya hivyo, ndipo mambo yalipobadilika.

FA wamemfungulia mashtaka Costa kwa makossa hayo mawili na kwa upande wa Gabriel itamlazimu kujibu mashtaka ya kuonyesha utovu wa nidhamu wa kujaribu kumpiga kwa nyuma mshambuliaji huyo kutoka nchini Hispania kitendo ambacho kilisababisha aonyeshwe kadi nyekundu.

Mbali na mashataka kwa wachezaji hao wawili, FA pia imezifungulia mashtaka klabu za Arsenal pamoja na Chelsea kwa kushindwa kuwatuliza wachezaji wao wakati wa mchezo huo na kujikuta wakiingia kwenye vitendo vya utovu wa nidhamu.

Costa amepewa muda wa kujibu mashtaka yanayomkabili kabla ya saa 12 jioni kwa saa za nchini England, ili hali Arsenal, Chelsea pamoja na Gabriel wanatakiwa kuwasilisha maelezo yao FA kabla ya saa 12 jioni siku ya al-khamis.

CCM: Waompenda Lowassa Wavue Magwanda
Malinzi Afunga Fainali Za Airtel Rising Stars 2015