Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kuwa na uhakika na uwepo wa viongozi wa chama hicho wanaokihujumu kwa kusaidia harakati za mgombea urais kupitia Chadema anaeungwa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa.

Akiongea katika mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya chama hicho, Abdallah Bulembo, aliwaambia wakazi wa Bukoba Vijijini kuwa wanazo taarifa za kuwepo viongozi hao ambao waliratibu mapokezi na mkutano wa Lowassa uliofanyika hivi karibuni mkoani Kagera.

“Msidhani hatufahamu…mikakati yote namna mnavyofadhili Ukawa na Lowassa tunafahamu, tenda tunawafahamu kwa majina,” alisema Bulembo na kuonya kuwa watu hao wasipojiondoa wenyewe wataondolewa na chama hicho baada ya Dk Magufuli kushinda.

Bulembo aliwataka viongozi hao kufanya uamuzi mapema na kuchagua kukitumikia chama hicho kwa uaminifu au kukihama mara moja kama wanapenda kufanya kazi na Ukawa.

“Anayempenda Lowassa na Ukawa avue magwanda ya CCM  awafuate huko huko. Hatutaki mtu ambaye mchana ni CCM usiku ni Lowassa,” alisema na kusisitiza kuwa CCM ni gari kubwa, wapo wanaoshuka na wanaopanda.

Kilio hicho pia kiliwasilishwa na mgombea urais wa chama hicho, Dk Magufuli wakati alipokuwa akiwahutumia wananchi katika jimbo la Muleba Kusini. Aliwataka wananchi hao kuachana na tabia za baadhi ya wanachama ambao hukihujumu chama hicho kwa kuwasaidia Ukawa.

Dk Magufuli aliwaomba wananchi hao kutomuangusha na kumchagua, “mimi nina moyo kama nyie, msiponichagua nitakwazika sana.”

Neymar Amuita Kiaina Philippe Coutinho FC Barcelona
FA Yawafungulia Mashtaka Costa Na Paulista