Yule komediani mtukutu wa Uingereza, ametoa mpya baada ya kuvamia mkutano wa waandishi wa habari aliokuwa akiendesha Rais wa FIFA, Sepp Blatter aliyetangaza kujiuzulu na kumwaga noti feki za dola.

Simon Brodkin, ambaye vipindi vyake vimekuwa vikimuhusisha mwanasoka Jason Bent na Lee Nelson, alivamia mkutano huo huku wengi wakiamini ni mmoja wa waandishi na kuanza kumwaga dola hizo za bandia kwa Blatter.

Aliendelea kumwaga fedha hizo akiashuria kumpa rushwa kufuatia sakata la rushwa linalowakabiri maafisa wa FIFA: “Hizi ni kwa ajili ya Korea 2026,” alisema, akimaanisha kuwa anamhonga Blatter ili aipe Korea uenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2026.
Hali hiyo ilimfanya Blatter abaki amepigwa butwaa kabla ya walinzi kuingia na kumtoa Brodkin. Hii ni kawaida ya Brodkin ambaye amekuwa akifanya hivyo sehemu mbalimbali.

Hivi karibuni alimvamia jukwaani Kanye West wakati akitumbuiza na yeye kuanza kutumbuiza.
Kabla ya hapo, aliwahi kutoa kali alipoungana na wachezaji wa timu ya taifa ya England akizuga naye ni mchezaji lakini akashitukiwa hatua ya mwisho wakati akikaribia kupanda ndege.

Fupa La Kibrazil Lamshinda Mourinho, Kulirudisha Alikolitoa
Wasanii Nane Wa Tanzania Watajwa Kuwania Tuzo Za AFRIMMA, Marekani, Diamond Aongoza