Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli amekutana na mwanamuziki Nguza Viking “Babu Seya” na wanae Johnson Nguza “Papii Kocha’, Francis Nguza na Nguza Mbangu walipokwenda Ikulu jijini Dar es salaam.

Familia ya mwanamuziki huyo imesema kuwa lengo kubwa la kukutana na Rais Dkt, Magufuli ni kumshukuru kwa kuwapa msamaha wa kifungo cha maisha Babu Seya na mwanae Papii Kocha walichokuwa wanatumikia toka wahukumiwe miaka 13 iliyopita.

“Yaani hapa ninafuraha kweli, sijui hata nisemeje, tumekuja kumshukuru Rais kwa kutupatia msamaha, na tumemuomba aturuhusu tuanze kufanya kazi,”amesema Babu Seya

 

 

Watoto 67 wakatiliwa na familia zao
Picha: Paka wa ajabu azaliwa, ana vichwa viwili na macho matatu