Paka wa ajabu aliyepewa jina la Bettie Bee aliyezaliwa akiwa na vichwa viwili, macho matatu na midomo miwili ameishi siku 16.

Bettie Bee alizaliwa Disemba mwaka jana nchini Afrika Kusini akimshangaza mtunzaji wake ambaye aliamua kutoa taarifa haraka kwa mtu  ambaye anafahamika zaidi kwa kufuga paka.

Kwa mujibu wa mahojiano maalum yaliyofanywa kwa njia ya barua pepe na gazeti la News Week, mtu aliyemtunza paka huyo alieleza kuwa alifanikiwa kukaa naye akiwa hai akiishi kama paka wengine, lakini alikabiliwa na ugonjwa wa pneumonia.

Alisema kuwa ugonjwa huo ulipelekea Bettie kudhoofika ghafla na baada ya siku 16 za maisha yake alikufa.

Alisema kuwa baada ya kugundua kuwa ana ugonjwa huo, alichukua hatua za matibabu lakini alijikuta akitapika kila alichokuwa anakula.

“Alikuwa anahangaika tangu mwanzo lakini nilifanya kila iwezekanavyo kuhakikisha anapona. Kwa siku 16 nilifanya kila liwezekanalo, nilifanya hivyo kila wakati, alistahili kuwa na maisha lakini bahati mbaya haikuwa hivyo,” alieleza kwenye mahojiano hayo.

Maelezo hayo yaliyochapishwa na gazeti hilo yaliwekwa pia kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook.

Familia ya Nguza Viking "Babu Seya" yatinga Ikulu
TCRA yawalima faini Star TV, Azam TV kuhusu uchaguzi wa madiwani