Mkongwe wa muziki wa HipHop hapa nchini Farid Kubanda maarufu kama Fid q amehairisha kwenda kufanya tamasha la MTV Base Show Case linalotarajiwa kufanyika nchini Afrika ya kusini tarehe 6 septemba mwaka huu kufuatia vurugu zinazoendelea nchini humo.

Msanii huyo aamesema kuwa vurugu zinazoendelea nchini humo zimechangia yeye kuhairisha kwenda kutumbuiza katika tamasha hilo.

Mkali huyo wa Mwanza ndie msanii wa kwanza kutoka Afrika mashariki kwenda kutumbuiza katika jukwaa la Big brother nchini Afrika ya kusini.

Katika mahojiano na  Millard Ayo amesema kuwa ‘sioni vibe ya kwenda kufanya show kwenye clouds ambayo inanitizama mimi kama foreigner ambae nimeenda kuchukua fursa zao’.amesema Fid Q

Aidha amesema hataki yeye kuwa sababu ya mtu kupata matatizo pindi atakapo toka kwaajili ya kuhudhuria tamasha atakalo kuwa anatumbuiza, amesisitiza kuwa amepata taarifa kutoka kwa mtu wake wa karibu kutoka Afrika Kusini kuwa kuna mpango wa msako wa mlango kwa mlango kwa raia wa kigeni nchini humo.

 

 

Madee kufuta nyimbo alizofanyia Afrika Kusini
Yanga yapinga Zahera kufungiwa mechi tatu