Mshambuliaji mpya wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC Gonzalo Higuain, amefichua siri ya kilichomuondoa kwenye klabu ya Società Sportiva Calcio Napoli (SSC Napoli) ambayo ilikubali kumuachia kwa dau la Pauni milioni 75 sawa na Euro milion 90.

Higuain, ambaye alipokelewa kwa furaha na mashabiki wa Juventus FC, siku mbili zilizopita mjini Turin, amesema rais wa SSC Napoli Aurelio De Laurentiis, alikua kikwazo cha yeye kuendelea kucheza soka mjini Naples.

Amesema ilikua ni vigumu kuendelea kuwa chini ya kiongozi huyo, kutokana na mahusiano kati yao kutokua mazuri, hali ambayo ilichagiza msukumo wa kutaka auzwe haraka iwezekanavyo.

Hata hivyo Higuain amemshukuru Laurentiis, kwa mazuri aliyowahi kumtendea tangu alipotua klabuni hapo miaka mitatu iliyopita na pia akatoa shukurani zake kwa mashabiki wa SSC Napoli ambao walionyesha kumpenda na kumthamini wakati wote alipokua akiishi mjini Naples.

“Ilinilazimu kufanya maamuzi ya kuondoka, lakini De Laurentiis alisababishwa kwa kiasi kikubwa kwa jambo hilo kutokea, lakini yote kwa yote sina budi kumshukuru na kuwashukuru mashabiki wa SSC Napoli kwa ushirikiano mkubwa walionionyesha.

Higuain alisajiliwa na SSC Napoli mwaka 2013, akitokea Real Madrid ya nchini Hispania na ameitumikia klabu hiyo ya Stadio San Paolo katika michezo 104 na kufunga mabao 71.

John Obi Akana Kuisaidia Timu Ya Taifa
Jurgen Klopp: Siwezi Kumsajili Mchezaji Kwa Milion 100