Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema kuwa hakuwahi kumuunga mkono aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa kama wengi wanavyoamini bali alikuwa akialikwa katika mikutano yake kufanya maombi.

Akiongea na Azam TV hivi karibuni, Gwajima alieleza kuwa yeye hakuwahi kumsapoti mtu binafsi ‘personality’ bali alikuwa anasapoti mabadiliko ya kweli na hadi sasa msimamo wake ni kuunga mkono mabadiliko ya kweli bila kujali mtu au chama.

“Watu wengi wanapenda kusema Unajua Gwajima alimsapoti Mheshimiwa Lowassa. Definition hii ni kubwa sana… kwa sababu mimi nilionekana kwenye mikutano ya Lowassa Arusha, nikaitwa kuomba… nikaomba. Na kwenye mkutano wa ufunguzi wa Ukawa Jangwani nikaitwa kuomba… nikaomba. 

“Na Dk. Slaa akaongea maneno ambayo yananihusisha mimi nikaenda kuya-confirm kwenye vyombo vya habari. Vitendo vile vitatu ndivyo viliitwa ‘unamsapoti Lowassa’. Lakini basically, nasapoti mabadiliko ya nchi. Sisapoti personality ya mtu. Sisapoti chama cha mtu. Nasapoti mabadiliko ya nchi.”

Video: Idris Sultan Atakuacha na 'Furaha' Jinsi alivyofunguka kwenye The Playlist
Ridhiwani Afunguka Kuhusu Tuhuma Za Ufisadi na Uhusika Sakata la Makontena