Msanii chipukizi kwenye kiwanda cha muziki wa bongo flava Anjella kutoka katika lebal ya muziki Konde Gang amefikisha zaidi ya wafuatiliaji 100,000 kwenye mtandao wa Youtube na kama ilivyo utaratibu, amepatiwa tuzo maalum ya pongezi kwa kufikisha idadi hiyo ya wafuatiliaji kupitia mtandao huo.

Kupitia mtandao wake wa Instagram ameweka picha kadha ambazo zinamuonyesha akiwa na tuzo hiyo iitwayo SILVER BUTTON AWARD kutoka

“Haikuwa kazi rahisi toka nimeianza safari yangu ya mziki rasmi Nimeuona upendo wenu wa dhati mashabiki zangu ambao mmejitolea muda wenu kufatilia kazi zangu Asanteni sana Upendo wenu umekuwa somo kubwa sana katika maisha yangu na hili limethibitika baada ya kufikisha Wafutiliaji 100,000 kwenye @youtube account yangu ( SILVER BUTTON AWARD ) Asante sana endeleeni ku Subscribe account ya @youtube usisahau ku Turn on” ameandika Anjella

Angella kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya Nobody ambao umefikisha jumla ya watazamaji 3.3M kwenye mtandao wa youtube ikiwa ni wiki tatu tu, tangu kuachiwa wimbo huo.

Kiongozi mbio za mwenge agoma kufanya ufunguzi wa zahanati
Kim apiga marufuku tamaduni za nje Korea Kaskazini