Nyota wa muziki wa bongo fleva Harmonize amevunja ukimya kuhusu mwenendo wa muziki wa bongo fleva na sababu zinazopelekea kukawia kwa mafanikio sawa na yenye kuonekana kwa wasanii wa mataifa mengine kama Nigeria na Afrika kusini.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Harmonize ambaye jina lake halisi ni Rajab Kahali amesema kuwa kabla ya mashabiki kuwashindanisha wasanii wa Afrika mashariki hasa wa Tanzania na wale wenye kutoka mataifa mengine yaliyofanikiwa kimuziki barani Afrika ni muhimu kuzingatia lugha ambayo wao wanatumia na ukubwa wa eneo ambalo lugha hiyo inazungumzwa.

Aidha Harmonize ameweka wazi kuwa ni njema kwa wasanii kutumia lugha ya kiswahili kwenye nyimbo zao ili kuitanga, lakini pia ni vyema kwa wao kutumia lugha ya kiingereza kwenye baadhi ya nyimbo ili kujaribu kulisogea soko la muziki nchini kwenye viwango vya kimataifa.

Buriani rapa Kiernan Forbes – AKA

“Asanteni Kwa Mapokezi Makubwa ya #SA huu wimbo hata msinge uthamini na kuupa nafasi kama ilivyo now pengine isingeniumiza nachukulia kama mwanzo wa safari yangu ya kukimbilia ndoto.

Imekuwa ni ndoto ya kila msanii kufanya matamasha makubwa na kujaza watu wengi kama wenzetu tunaolinganishwa nao wa west africa hadi kupelekea tunatukanwa tukifanya show na kupata mashabiki wachache nchi za nje ya Africa.

Ukweli mchungu ni kwamba sisi Africa mashariki tupo wachache, ingawa tunapendana sana kulinganisha na wenzetu West !!! Lakini wachache hao hao karibia nusu wanaongea kizungu na inakuwa rahisi kuzipenda na kuziimba nyimbo zao, wenzetu wao ni wengi na pamoja na wingi wao hata robo hawajui tunachokiongea na kukiimba, tatizo huanzia hapo”. Amesema Harmonize na kuongeza

Diamond, Ali kiba, Harmonize, na Zuchu

“Ni ngumu pia wimbo usipo Hit nyumbani kwako kuwa Hit Kwa Wenzio, ushauri wangu TUIPENDE LUGHA yetu tujivunie tuimbe na kuipamba maana LUGHA Yetu ndio fahari yetu, ndio utamaduni wetu ila isifikie pahala tukadhani mataifa yote yanaelewa hii lugha adhim.

Nadra sana kutokea wimbo ukawa maarufu mataifa mengine inatokea Mara Chache, tena ni pale producer akipiga mdundo mkali na sio maneno naipongeza sana Basata kwa jitihada za kutafuta mdundo wa taifa pengine nasisi Tukapata sound ya kututambulisha kama Ilivyo kwa wenzetu South Africa”.

“Good Basata tuimbeni tujivunie tamaduni zetu Ila tukipata nafasi tuwe tunaimba hii LUGHA mara Moja Moja Sio Mbaya ninaimani itasaidia kutangaza tamaduni zetu na kupelekea hata mataifa mengine Kuufuatilia muziki wetu na kujifunza hata lugha zetu pamoja na tamaduni zetu.

Maana nyimbo za namna hii zitawapa mwangaza wakujua tunavipaji kiasi gani Shukrani sana wote mnao sapoti nyimbo za hivi pamoja na nyimbo nyingine, na wasio sapoti basi wasijiulize kwanini hatuendi International”. Amesema Harmonize.

Burna Boy, Davido, Wiz Kid

Pamoja na hayo Konde boy amewaasa mashabiki wa muziki nchini kuacha kuwashindanisha wasanii wa Tanzania na wasanii kutoka nchini Nigeria kutokana na kile anachodai kuwa mafanikio yao yanachangiwa na lugha wanayotumia kuwa yenye kusikilizwa na kueleweka na idadi kubwa ya watu duniani ukilinganisha na Kiswahili.

“Muache pia kutushindanisha na wakina Burnaboy & Davido, Wizkid kwa sababu wanasikilizwa na Kueleweka wanacho Kiongea Karibia na Dunia nzima.

Thank me Later, REMA, RUGER na OMARAY wametupita Mbali Lol wanalipwa pesa nyingi kwa show Kuliko Msanii yeyote wa Africa Mashariki Maana Wanasikilizwa eneo kubwa”. Amesema Harmonize

Tunawathamini wazalishaji Chumvi: Dkt. Kiruswa
Wafugaji waliojeruhi wakulima kusakwa