Kocha mpya wa timu ya taifa ya Moroco, Herve Renard ametaja kikosi chake cha kwanza tangu alipotangazwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi mwezi uliopita.

Renard, aliyekiwezesha kikosi cha Ivory Coast, kutwaa ubingwa wa Africa mwaka 2015, ikiwa ni miaka mitatu baada ya kuiwezesha Zambia kufanya hivyo, alitangazwa kuwa kocha mkuu wa Morocco, akichukua nafasi ya Badou Zaki.

Morocco wanatarajia kupambana na Cape Verde, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika za mwaka Africa 2017, utakaochezwa mwishoni mwa juma lijalo.

Kikosi hicho kamili kilichotajwa na kocha huyo kutoka nchini Ufaransa upande wa walinda mlango ni Mounir El Kajoui (Numancia), Yassine Bounou (Real Zaragoza), Abdelali M’Hamdi (RSB Berkane)

Safu ya Ulinzi ni Mehdi Benatia (Bayern Munich), El Kaoutari (Reims,), Issam Chebake (Le Havre, , Achraf Hakimi (Real Madrid B,), Nabil Dirar (Monaco), Marouane Da Costa (Olympiakos,), Mohamed Oulhaj (Raja Casablanca), Achraf Lazaar (Palermo), Hamza Mendyl (Lille), Romain Saïss (Angers,)

Viungo ,Karim El Ahmadi (Feyenoord), Mounir Obbadi (Lille), Younes Belhanda (Schalke,), Abdelaziz Barrada (Marseille), Omar El Kaddouri (Napoli)Fayçal Fajr (Deportivo La Coruna), Youssef Aït Bennasser (Nancy), Nordin Amrabat (Watford), Mehdi Carcela-González (Benfica), Hakim Ziyech (Twente,), Mbark Boussoufa (Gent,), Walid El Karti (WAC)

Khalid Boutaïb (GFC Ajaccio,), Oussama Tannane (Saint-Etienne), Badi Aouk (HUSA), Morad Batna (FUS), Yacine Bamou (Nantes), Youssef El Arabi (Granada) Youssef Naciri (Malaga,), Abdelghani Mouaoui (IRT), AbderRazak Hamadellah (El Jaish)

Picha: Bibi harusi Ampiga bwana harusi mbele ya waalikwa, Siku ya wanawake duniani
Man Utd Yashindwa Kufurukuta Anfield