Mgombea Urais kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton amegundulika kuwa na ugonjwa wa homa ya mapafu baada ya kuugua katika tukio la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.

Daktari wake Lisa Bardack amesema kuwa bi Clinton amekutwa na ugonjwa huo tokea Ijumaa iliyopita

Amesema pia Clinton aliongezeka joto na kuishiwa na maji mwilini katika tukio hilo la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.

Clinton aliondoka mapema katika tukio hilo huku picha  zikimuonesha akisaidiwa na msaidizi wake, huku akitaka kuanguka alipokaribia kwenye gari, lakini baadae bi clinton alitokea kwenye nyumba ya mwanae na kuwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuri

Awali mgombea Urais kupitia chama cha Republican Donald Trump alionesha wasiwasi juu ya afya ya hasimu wake na kusema clinton afya yake ni dhaifu.

Katika shughuli hiyo majina karibu elfu tatu ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11 yalisomwa

Diwani apigana ngumi na Mwenyekiti kumgombea Ofisa Mtendaji
Ibada ya Hijjah Yafikia Kilele Chake Mlima Arafat