Serikali nchini Namibia, imetangaza kifo cha mtu mtu mmoja kilichotokana na homa ya kuvuja damu aina ya Crimean-Congo na kusababisha kutoa tangazo la mlipuko wa ugonjwa huo, ambao pia unajulikana kama homa ya Congo, ukliwa na kiwango cha juu cha vifo hadi asilimia 40.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani – WHO, imeeleza kuwa kesi moja inachukuliwa kama mlipuko huku Mkurugenzi Mtendaji wa Wizara ya afya, Ben Nang’ombe akisema ugonjwa huo unasambaa kwa kung’atwa na kupe, na hivyo unaweza kuchukuliwa kama mlipuko wa ndani.

Aidha, imesema ilichukua maelezo kwa mtu aliyeambukizwa ambaye alipelekwa kliniki katika mji wa mashariki wa Gobabis akiwa na dalili za ugonjwa huo, ambaye alisema anahisi homa, maumivu ya misuli, kizunguzungu, kupata shida kutazama eneo lenye mwanga na kichefuchefu.

Hata hivyo, baadae mtu huyo aliwekwa karantini katika hospitali ya mji mkuu wa nchi hiyo, Windhoek na inaarifiwa kuwa alifariki muda mfupi baadaye.

Neville, Carragher wataja vikosi EPL 2022/23
Rada za Munich zamnasa Declan Rice