Kampuni ya Yono imeifunga Hotel ya Blue Pearl kwa kudaiwa kodi na Ubungo Plaza kiasi cha shilingi billioni 5.7 tangu mwaka 2014.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Scholastika Kevela, ambapo amesema kuwa Hoteli imefungwa kutokana na kudaiwa kodi na Ubungo Plaza kwa muda mrefu.

“Tunafunga na kukabidhi kwa mmiliki, na shughuli hapa hazitaendelea tena hadi awe amelipa kodi hiyo kiasi cha shilingi bilioni 5.7 kwa mmiliki ndipo atakapo ruhusiwa kuendelea na shughuli zake,”amesema Kevela

Hata hivyo baadhi ya wateja waliokuwemo katika hotel hiyo, akiwemo Masoud Masoud amelalamikia kitendo hicho akidai kuwa ametoa hela nyingi na alikuwa akae wiki mbili na familia yake, lakini ameingia jana tu, huku kuwa huo ni usumbufu.

Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu mchakato wa Katiba Mpya
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Zimbabwe akimbia, Mke wa Mugabe atajwa kumrithi