Shirikisho la riadha duniani IAAF limempiga marufuku Papa Massata Diack kutojihusisha na shughuli zozote za riadha maisha yake yote.

Papa Diack alikuwa mshauri wa masuala ya mauzo wa shirikisho hilo.

Ni mwanawe mkuu wa zamani wa IAAF Lamine Diack.

Alikuwa ameshtakiwa kwa kukiuka maadili ya shirikisho hilo.

Mkuu wa shirikisho la riadha la Urusi Valentin Balakhnichev na kocha Alexei Melnikov pia wamepigwa marufuku kutojihusisha na riadha maisha yao yote.

Mashtaka dhidi yao yanahusiana na malipo ya

£435,000 ($633,000) ambayo mshindi wa zamani wa London Marathon Mrusi Liliya Shobukhova alilipa ili kuondolewa tuhuma za kutumia dawa zilizoharamishwa.

“Kuwapa adhabu ya chini kushinda hiyo kutakuwa ni kudunisha uzito wa makosa waliyotenda,” kamati ya maadili ya IAAF imesema.

Mwezi uliopita, Papa Massata Diack, anayeishi Senegal, alisema anakanusha madai yote ambayo waendesha mashtaka nchini Ufaransa walikuwa wamewasilisha dhidi yake.

David Moyes Akiri Kuitamani Man Utd
Visiki Vya Afrika Kupambanishwa Hii leo

Comments

comments