Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amefanya ziara katika bandari ya Dar es salaam leo Januari 3, 2018 kwa lengo la kukagua magari 119 ya Jeshi hilo ambayo yameshawasili bandarini hapo.

Magari hayo ni miongoni mwa magari 777 yaliyoagizwa na Jeshi hilo, ambapo IGP Simon Sirro akiwa ameongozana na baadhi ya maofisa wa Jeshi hilo amekagua baadhi ya magari hayo ambayo ni kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kipolisi.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 4, 2018
Video: Majaliwa aomboleza msiba wa mke wa Naibu Waziri Kangi Lugola