Katika kusherekea siku ya kuzaliwa ya Aunty Ezekiel, Diamond Platinumz alifunguka na kuwachambua watu wenye tabia ya kuingilia mahusiano ya watu wengine hasa pale wanapokuwa wamegombana.

Diamond amesema kuwa wapenzi wanapokuwa wamegombana ameshauri ni heri watu wengine kukaa pembeni na kuwaacha wawili hao kumaliza tofauti zao kuliko kutia mafuta kwenye moto na kuchochea ugomvi wa wawili hao ukijua hawatakuja kupatana au kufurahia tofauti zao.

Maneno hayo yamekuja baada ya wawili hao Moses na Aunty Ezekiel kugombana na kufikia hatua ya kuachana kwa takribani mwaka sasa na hatimaye katika kusherekea siku ya kuzaliwa ya Aunty wawili hao wameonesha wazi kuwa wamerudiana.

Diamond amefunguka na kusema tangu kugombana kwa wawili hao alijua siku kama ya leo ingefika ya kupatana kwao kwani alikuwa anatambua dhahiri kuwa wanapendana na yeye kama rafiki wao alikuwa katika wakati mgumu sana kutokana na mahusiano ya karibu aliyonayo kwa Anty na Moses mwenyewe.

”Mkiona wapenzi wanagombana tembeeni, Mimi wakati tofauti ya Aunty na Moze ilivyokwepo nilikaa pembeni sababu nilijua siku kama leo ingefika, hawa ni familia wanamtoto na mtoto wao wanampenda na sisi tunampenda nyie msisherekee kutengana kwao, msisherekee migombano yao, tuwaombee Mungu, kugombana kupo si tunagombana na wazazi wetu, mimi nina gombana na mama yangu na ninampenda kweli lakini yanakaa yanaisha, kwahiyo watu muache kuwa vimbelembele kwenye mahusiano ya watu” amesema Diamond.

Aidha, Diamond alitumia nafasi hiyo kumsema jamaa ambaye alikuwa kwenye mahusiano na Aunty kipindi ambacho hakuwa pamoja na Iyobo jamaa huyo alifahamika kwa jina la Alfo Alfo kwenye mtandao wa kijamii wa instagram Nasseb amesema hii ndio WCB akidai kuwa wao huwa hawafeki mapenzi kwamba wakipenda wanapenda kweli.

”Yule bwana mdogo aliyekuwa anapostiwa instagram yumo humu ndani najua saiv atakuwa na hali  mbaya, mwambieni hii wasafi, WCB, halafu sisi hatufeki mahusiano tunapenda, Mose anampenda Aunty na Aunty anampenda Mose”. amesema Diamond.

Aidha alitoa vibunda viwili vya pesa ambavyo alimkabidhi moze iyobo kama zawadi yake kwenye siku siku hiyo ya kuzaliwa mara baada ya kumtaka Aunty achague zawadi anayotaka kutoka kwake na kusihia kumwambia amchopie hela, na zoezi hilo lilifanywa na Moses Iyobo akilisindikiza na shoo ndogo ya dance.

Mvua yakwamisha Safari za Treni
AFRIMMA 2019: Ommy Dimpoz awabwaga Diamond, Ali Kiba, Harmonize, Kenzo...