Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amekemea   tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililo tolewa  kupitia vyombo vya habari  kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa na kusainiwa na Jaji Francis Mutungi imebainisha kuwa tamko hilo linaenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu 9 (2) (c) inayo kataza chama cha siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa.

“Nimepokea kwa masikitiko tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa  kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini. Tamko hilo limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa amani” Ilisema taarifa hiyo

Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa kifungu cha 9(2) (f) kinakataza chama cha siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au ikapelekea kutokea uvunjifu wa amani.
Aliongeza kuwa kanuni ya 5(1) (d) inakitaka kila chama cha siasa kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni uongo. Kuhusu mtu yoyote au chama cha siasa chochote.
Katika taarifa yake Jaji Mutungi amesema kutokana na Kanuni hizo tamko la CHADEMA ni ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.

Aidha, hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani (civil disorder).Alisema

Natumia fursa hii kukemea tamko hilo hadharani, kwa mujibu wa kanuni ya 6(2) ya Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Pia nawaasa CHADEMA wasiendeleze tabia hii.

Jaji Mutungi ametoa rai kwa  Viongozi wa Vyama vya Siasa  waonyeshe ukomavu katika medani za Siasa badala ya kujikita katika vitendo, kauli au matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au kufarakanisha Umma na Serikali yao.

CHADEMA wameitangaza siku ya tarehe mosi Septemba kama ni siku maalum kwao kufanya mikutano nchi nzima ikiwamo maandamano ambapo ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa zitahusika.

Video: Makonda amekuja na mkakati mwingine wa Dar es salaam
Waziri Mkuu Aitaka Halmashauli Ya Temeke Kuondoa Wafanyakazi Wa Mkataba