Wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) wanatarajia kupiga kambi Uganda kwaajili ya matayarisho ya mchezo wao dhidi Gaborone United kutoka Botswana utakaochezwa siku ya Jumapili ya tarehe 14/2/2016 saa 10.30 za jioni katika kiwanja cha Amani.

Mtandao huu umezungumza na Sadu Ujudi ambae ni katibu wa timu hiyo akisema kuwa wanatarajia kwenda Tanzania Bara kupiga kambi fubi kisha wataelekea moja kwa moja Uganda.

Ujudi aliweka wazi mpaka michezo yao ya kirafiki watakayocheza Uganda.

“ Tumejipanga vizuri sisi JKU, tutakwenda bara kupiga kambi fupi, kisha tutakwenda Uganda kucheza michezo mitatu ya kirafiki na katika michezo hiyo tumepangiwa kucheza tarehe 31 mwezi huu wa January, kisha tutacheza tarehe 2 Februari na  Sports Club Villa na mechi ya mwisho tutacheza tarehe 4 Februari na mabingwa wapya wa kombe la Mapinduzi timu ya URA, ambapo tulipokutana mwaka huu Zanzibar walitufunga 3-1, lakini tutawalipa huko huko kwao”. Alisema Ujudi.

Hayo ni Maandalizi ya Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho kati ya JKU ya Zanzibar dhidi ya Gaborone United kutoka Botswana itachezwa siku ya Jumapili ya tarehe 14/2/2016 saa 10.30 za jioni katika kiwanja cha Amani.

Pambano hilo nalo litachezeshwa na mwamuzi George Gatogoto kutoka Burundi akisaidiwa na Gustava Baguma,Willy Habimana,Thierry Nkurunziza wote kutoka Burundi.

Kamisaa wa mchezo huo ni Andrea Almas kutoka Sudan ya Kusini.

Na Mchezo wa marejeano utafanyika huko Botswana tarehe 26/2/2016 saa 2.00 za usiku kwa saa za Botswana ambapo sawa na saa 3.00 za usiku kwa saa za hapa nyumbani.

Serikali yawatetea Lowassa, Sumaye
Mbowe aeleza watakachofanya kuzuia mpango wa Nape kuhusu TBC