Gwiji wa soka nchini Uholanzi na klabu ya Barcelona, Hendrik Johannes Cruyff, amemkosoa meneja wa klabu ya Mana Utd, Louis van Gaal kwa kusema hatumii mfumo unaostahili.

Cruyff, ambaye ana uhusiano wa karibu wa Van Gaal, ameyasema hayo alipofanyiwa mahojiano maalum na kituo cha televisheni cha Sky Sports News HQ cha nchini England.

Cruyff ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha FC Barcelona, amesema Van Gaal amekua akikosea sana katika mfumo wa uchezaji ambao anautumia kikosini kwake kwa sasa, na matokeo yake amekua akijikuta anapata wakati mgumu wa kuambulia sare, kufungwa ama kushinda kwa tabu.

Amesema Van Gaal, anapaswa kurejesha mfumo wa kikosi chake kumiliki mpira na kucheza kwa kujiamini wakati wote, na si mambo yanavyoonekana sasa ambapo kumekua na wachezaji wanaolengwa kwa kupigiwa mipira mirefu.

Amesema yeye ni muumini wa soka la pasi la kumiliki mpira na ndivyo wachezavyo Barcelona mpaka sasa, hivyo haoni sababu kwa Van Gaal kuacha mfumo huo ambao aliwahi kuutumia akiwa Camp Nou pamoja na FC Bayern Munich.

Johan Cruyff, amelazimika kusema jambo hilo baada ya kukerwa na soka walilocheza Man utd mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Arsenal ambao walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri kwenye uwanja wa Emirates.

Biram Diouf Afiwa Na Mama Mzazi
Stars Yajiweka Sawa, Yaitandika Malawi