Mgombea nafasi ya uraisi ndani ya FC Barcelona, Jordi Farre ameweka wazi kuwa, akipata ridhaa ya kuchaguliwa na kuwa Rais atahakikisha anamshawishi nahodha na mshambuliaji wa kikosi cha klabu hiyo Lionel Messi, anabaki klabuni hapo na kusaini mkataba mpya.

Kutokana na hali ya mkataba wa sasa wa Messi, mshambuliaji huyo kutoka nchini Argentina atakuwa mchezaji huru mwezi Juni 2021, na hadi kufika mwezi ujao tayari atakuwa na uwezo wa kuanzisha mazungumzo na klabu nyingine yeyote duniani.

Farre, amesema atakua na kila sababu ya kufanya hivyo ili kuboresha mazingira ya klabu hiyo ambayo bado inamuhitaji Messi katika kipindi kingine, kwa mipango ya kufanikisha mazuri huko Camp Nou.

Amesema haoni sababu suala la mshambuliaji huyo kuzungumzwa juu juu, huku ikifahamika itakapofika mwishoni mwa msimu huu ataondoka, baada ya mipango ya kulazimika kuuzwa mwanzoni mwa msimu huu kufeli.

“Nitalifanyia kazi suala hili. Messi na klabu ni sehemu ya klabu, na taswira yake pamoja na Barcelona zinatakiwa kuungana milele. Ni mechezaji bora kwenye historia ya soka, tunapaswa kumpa dili nono.” Amesema Jordi Farre

Messi alishinikiza kuondoka klabuni hapo wakati wa usajili wa majira ya kiangazi, huku klabu za Manchester City (England) PSG (Ufaransa) na Inter Milan (Italia) zilikua zinatajwa kuwa mstari wa mbele kumsajili.

Dkt. Gwajima awataka Viongozi Wizara ya Afya kuongeza ufanisi
Lema, familia yake wakimbilia Canada

Comments

comments