Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.
Aidha, Jenerali Venance S. Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Meja Jenerali James M. Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.
Luteni Jenerali James M. Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance S. Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa hapo baadaye.

Merkel amsisitizia Erdogan kuheshimu uhuru
AFCON 2017: Cameroon Yaifuata Misri Fainali