Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa kuna umuhimu wa kulinda uhuru wa maoni ya wananchi.

Ameyasema hayo alipokuwa katika mazungumzo na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alipoitembelea nchi hiyo kwa mara ya kwanza tangu kufanyika jaribio la mapinduzi.

Aidha, Wakiwa katika mkutano wa pamoja mbele ya waandishi habari, Erdogan amesema yeye na Kansela Merkel wamezungumzia kuhusu yanayoendelea nchini Syria, Iraq na bahari ya Aegean.

Erdogan amesema aligusia pia suala la ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi, mgogoro wa wahamiaji pamoja na uwezekano wa kupiga hatua za pamoja katika vita vinavyoendelea nchini Syria.

Naye Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amemsisitiza Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, kuheshimu  maadili ya kidemokrasia ya uhuru wa kujieleza, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini humo tokea jaribio lamapinduzi ya kijeshi la mwezi Julai.

Merkel amewaambia waandishi habari kwamba ameahidi kumuunga mkono Erdogan katika jitihada zake za kuwasaka waliohusika na uasi huo wa kijeshi. Hata hivyo Merkel amesisitiza kuwa uhuru wa kujieleza pamoja na tofauti za misimamo ya kisiasa yasivurugwe.

Ujerumani imekuwa ikionyesha wasiwasi juu ya Uturuki na kusema kwamba inatumia hatua kali kuulenga upinzani wa kidemokrasia pamoja na wanahabari, na hilo linaweza kuuweka mashakani uhusiano wa nchi hizo mbili.

Magazeti ya Tanzania leo Februari 3, 2017
JPM afanya uteuzi wa mkuu wa majeshi