Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo amemteua Mama Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taariza za uteuzi huo wa Mama Salma ambaye ni mke wa aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, zimetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mama Salma ataapishwa hivi karibuni kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati akiwa ‘First Lady’, Mama Salma aliwekeza nguvu zake katika kusaidia juhudi za kuwakwamua wasichana na wanawake kwa ujumla katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwa ni pamoja na afya na uchumi.

Mama Salma pia alionesha uwezo mkubwa wa kisiasa hasa wakati wa kampeni mbalimbali za kisiasa, ambapo alikinadi vyema Chama Cha Mapinduzi.

 

Magazeti ya Tanzania leo Machi 2, 2017
Polisi Arusha wakamata Bunduki 10 zikiwemo SMG, Risasi 59