Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Magufuli amesema kuwa siasa sio ugomvi.

Ameyasema hayo mara baada ya kuchaguliwa kuendelea kukiongoza chama hicho mjini Dodoma, ambapo ameibuka na ushindi.

Amesema kuwa Tanzania ni ya wote hivyo ni vyema kwa vyama vya siasa kujenga hoja zitakazojenga misingi imara kwa wananchi hasa katika nyanja za maendeleo.

“Siasa sio ugomvi, Tanzania hii ni ya kwetu tushindane kwa hoja zenye mashiko ambazo ztawajenga wananchi katika kuwamahasisha katika shughuli za maendeleo,”amesema Rais Dkt. Magufuli

 

ANC yapata mwenyekiti mpya, Mama Zuma ‘apigwa mtama’
LIVE DODOMA: Mkutano mkuu maalum wa CCM Taifa