Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amewaeleza watumishi wote (isipokuwa wale waliozuiliwa na Waziri Mkuu), kuwa wanapaswa kwenda likizo ya sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya kwa ajili ya kufurahia pamoja na ndugu na familia zao kwa ujumla.

Rais Magufuli, ametoa kauli hiyo hii leo Desemba 24, 2020, wakati akiwatakia heri ya sikukuu hizo watumishi wote, mara baada ya kumuapisha Kamishna wa Maadili aliyemteua hapo jana, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi, Ikulu ya Chamwino Dodoma.

“Wale mtakaoweza kusafiri kuwaona ndugu zenu ni ruksa siku mbili tatu au tano, kwenda kumuona mama yako si vibaya, hakuna dhambi kufika nyumbani, wengine mtaenda kufanya matambiko, isipokuwa wale waliouzuiliwa na Waziri Mkuu, nafikiri ni wakurugenzi na watu wengine wanaotakiwa kuwajibika ili shule zitakapofunguliwa kuwepo na madarasa, lakini wengine Ma DAS, DC, RC ni lazima mjipange ili ofisi msiziache wazi”, amesema Rais Magufuli.

Awali Rais Magufuli akizungumza, alisisitiza suala la usiri wa fomu zinazojazwa na watumishi wa umma, na kwamba hazitakiwi kurejeshwa kwa njia ya mtandao na badala yake zipakuliwe tu na kisha mhusika azirudishe sehemu sahihi.

Messi aichua siri ya kushindwa kung'aa La Liga
JPM aitaka tume ya maadili kukaa chonjo na mtandao