Mkali wa Sorry, Justin Bieber ameeleza sababu zilizopelekea yeye na Selena Gomez kushindwa kuwa pamoja na kuanzisha familia kama zilivyokuwa ndoto zao.

Akiongea katika kipindi cha The Bert Show, Bieber ameeleza kuwa walihitaji muda wa kukua lakini baada ya kufikia umri husika walijikuta hawako pamoja tena.

“Nilitaka tu awe na furaha. Ninampenda. Sisi ni marafiki. Tulihitaji muda wa kukuwa na tulikuwa tunafikiri kama… ‘labda tutarudiana siku za usoni’. Lakini tukaishia kuchukua muda mrefu na tukaanza kukua tukiwa mbalimbali na hatuko kama tulivyokuwa tena,” alisema Bieber.

 

Ali Kiba adai Davido alitamani kufanya naye Collabo
Yaliyojili leo Mahakama Kuu, Kesi ya Lembeli Kupinga Ubunge wa Kishimba