Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara inaelekea ukingoni. Ligi hiyo itakayotoa washindani watatu wapya katika ligi kuu msimu wa 2016/17, imegawanywa katika makundi matatu na kila mshindi wa kundi atapanda moja kwa moja VPL msimu ujao.

KUNDI B:

Mchuano mkali unaendelea katika kundi B, matajiri wa Geita chini ya kocha kijana Suleimani Matola, timu ya Geita Gold Sport inahitaji kushinda walau mchezo mmoja na kutoa sare mechi mbili kati ya tatu zilizobaki ili kufuzu kwa mara ya kwanza katika ligi kuu.

Geita Veterani’ jina la zamani la Geita Gold inaongoza kundi ikiwa na pointi 24 ikifuatiwa kwa karibu na ‘Maafande’ wa Polisi Tabora wenye pointi 21 katika nafasi ya pili.

JKT Oljoro ilichapwa 2-0 na Mbao FC ya Mwanza wikendi-jana inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na alama 19.

Mbao inafuatia ikiwa na pointi 15 wakati matajiri wa mafuta kutoka mkoani Kilimanjaro, Panone FC chini ya mwalimu Fred Felix Minziro wakiwa nafasi ya 5 na pointi zao 14 (pointi 10 nyuma ya Geita Gold)

Rhino Rangers ya Tabora imekusanya pointi 11 na huku kila timu ikiwa imesalia na michezo bila shaka ‘Wanajeshi’ hao watapaswa kupambana kutoshuka daraja sambamba na ‘Wanausalama wenzao’ Polisi Mara FC yenye pointi 9 na JKT Kanembwa ya Kigoma yenye pointi 3 katika nafasi ya mwisho ya kundi.

Maafande Wa Ruvu Shooting Warejea Ligi Kuu
Mtarajiwa Wa Kundi C Daraja La Kwanza Bado Kitendawili