Kufuatia ajali ilyosababishwa na uzembe wa madereva wa kampuni ya city boy na kusababisha vifo vya watu 30 na majeruhi,  Mamlaka ya usafiri tanzania SUMATRA imefungia kampuni hiyo kufanya huduma za usafirishaji kwa muda usiojulikana.

Kamanda wa jeshi la polisi usalama barabarani Mpinga  amesema wakati akiongea na wanahabari apo jana kuwa uzembe ulisababishwa na city boy sumatra imechukua hatua  kwa kampuni hiyo yenye mabasi 12 kutofanya usafirishaji kwa muda usiojulikana ikiwa ni sambamba na kampuni ya mohamed trans kwa kusababisha ajali nakuharibika mara kwa mara

Akizidi kueleza kamanda mpinga amesema mtindo wa kusalimiana wa madereva wa city boy uliosababisha ajali ni wa ajabu kwani jeshi la polisi halijawahi kukutana na malalamiko ya aina hiyo kwa abiria na kwamba kuanzia sasa jeshi la polisi litatia mkazo katika suala hilo.

Hata hivyo kamanda mpinga amesema kuwa mpaka sasa dereva mmoja ws city boy amekwisha kamatwa akiwa amevunjika miguu na kwamba dereva mwingine bado anatafutwa na kuna dalili za kumkamata.
“Tukiwakamata upelelezi utafanywa na baada ya hapo watafikishwa mahakamani mara moja kwa shtaka la kuua bila kukusudia”amesema Mpinga

Kutokana na ajali nyingi zinaonesha kuwa ajali nyingine husababishwa na madereva wakiwa wamelewa  Kamanda Mpinga amesema vifaa vya kupima ulevi kwa madereva ni vichache hivyo kufanya kuwa na changamoto katika kulidhiti hilo kwa asilimia kubwa

Oscar Pistorius atupwa jela Miaka 6 kwa kumuua mpenzi wake
Video: TRA - Mizigo haitozwi huduma Bandarini tu