Kufuatia Kesi ya uhujumu uchumi kwa kutoboa bomba la mafuta inayomkabili mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia, (Tazama), Samwel Nyakirang’ani (63), na wenzake sita imegonga mwamba mara baada ya  Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Thomas Simba kutohudhuria mahakamani siku ya leo na kupelekea kesi hiyo kusogezwa mbele.

Hivyo kwa maelezo ya Hakimu shahidi amesema, kesi hiyo imehairishwa mpaka 22, Machi 2018 ambapo shauri lao la dhamana litasikilizwa, mbivu au mbichi juu ya dhamana hiyo kufahamika.

”Mheshimiwa Hakimu Washtakiwa wote wapo hapa Mahakamani na kesi imekuja kwa ajili ya uamuzi wa dhamana dhidi ya washtakiwa na upande wa Jamhuri tupo tayari kuendelea” amesema Wakili Mkuu wa Serikali Peter Maugo.

Aidha washtakiwa wamefunguliwa kesi hiyo kwa makosa makuu matatu ya uhujumu uchumi kwa kuunganisha bomba la mafuta ya dizeli kinyume na sheria.

Mbali na Samwel, washtakiwa wengine ni  Nyangi Mataro (54), mwalimu wa shule ya msingi, wengine ni mfanyabiashara, Farijia Ahmed (39), Kristomsi Angelus (25), Fundi ujenzi Pamfili Nkoronko (40), na Hunry Fredrick (38).

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani mnamo januari 16, 2018 na kusomewa shitaka juu ya uhujumu uchumi baada ya kufanya wizi wa mafuta kinyume na sheria kwa kujiunganishia bomba la mafuta kutoka njia kuu na kufanya wizi wa mafuta hayo aina ya dizeli.

Agundua ana ujauzito nusu saa kabla ya kujifungua
Makamu wa rais awahimiza wanawake kuchangia maendeleo