Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuzindua kituo kipya na cha kisasa cha michezo baadaye mwezi huu kitakachoitwa Jakaya M. Kikwete (JMK PARK) kidongo chekundu jijini Dar es salaam.

Kituo hicho kitakuwa ni cha kwanza cha aina yake nchini, chenye kulenga miongoni mwa mambo mengi kuanzia kulea wanamichezo tangu wakiwa wadogo.

Kituo hicho kitafunguliwa kwa umma kwa mara ya kwanza Jumamosi ya Oktoba 29,2015, na hivyo kukiwezesha kuanza rasmi shughuli zake.

Shughuli kubwa ikiwa ni kulea watoto wa Kike na Wakiume kwa kupitia michezo.

Utaupenda Ujumbe Wa Zari Kwa Diamond Kwa Ajili Ya ‘Birthday’ Yake Leo
Mgombea Ubunge Atekwa, Watekaji Watoa Masharti