Nahodha wa mabingwa wa kombe la ligi nchini England (Capital One Cup) Manchester City, Vincent Jean Mpoy Kompany amesema huwa hajisikii furaha linapokuja suala la kikosi chao kushindwa kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita, mawazoni mwake.

Kompany amesema jambo hilo humuuma kila linapomuijia mawazoni mwake na wakati mwingine hufikia hatua ya kujutia kwa nini walishindwa kukamilisha mpango huo, ambao ulionekana kuwa katika njia sawia kwa Chelsea ambao walitawazwa kuwa mabingwa chini ya Jose Mourinho.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 29, amefunguka juu ya suala hilo siku moja baada ya vijana ya Manuel Pellegrini, kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Capital One Cup, kufuatia ushindi wa changamoto ya mikwaju ya penati walioupata dhidi ya majogoo wa jiji Liverpool, baada ya kufungana bao moja kwa moja ndani ya dakika 120.

Amesema walikua na kila sababu ya kutimiza lengo la kutetea ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini England kutokana na kuwa na kikosi bora ambacho kilifanikiwa kupambana wakati wote, lakini changamoto kadhaa ambazo walikutana nazo ziliwakwamisha na kujikuta wakiambulia patupu.

Hata hivyo Kompany amedai kwamba pamoja na chikwa kuuma juu ya jambo hilo, bado hujipa matumaini ya kuamini soka ni mchezo wa makosa na wakatyi mwingine hujiaminisha kwamba nafasi ya ubingwa kwa Man city bado ipo katika misimu kadhaa ijayo.

Nadir Haroub Shakani Kuwavaa Azam FC
Guus Hiddink Ang'aka Kuhusu Ratiba Ya FA, Champions League