Kama kuna mtu aliyezipokea kwa uchungu taarifa za kutemeshwa kibarua kwa kocha Rafael Benitez,  ni mmojawapo, hakupendezwa hata kidogo kusikia bosi wake huyo amepigwa chini.

Sio kutopendezwa tu na hatua hiyo, bali ameweka bayana kuwa, tangu siku hiyo amejikuta hana furaha kabisa na viunga vya Santiago Bernabeu.

Benitez ametsemeshwa mzigo mapema Jumatatu jioni na mara moja klabu ya Madrid imemtangaza Zinedine Zidane kuwa ndiye anayerithi mikoba yake.

Bale ambaye hana msimu mzuri ndani ya Madrid kwani ameifungia timu hiyo mabao saba tu katika mechi sita alizopangwa katika La Liga.

real

Sky Sports linaripoti kuwa Bale ni kati ya wachezaji waliokuwa wanaamini Benitez ndiye kocha sahihi na kwamba kuondoka kwake ni kama vile anaongeza ufinyu wa nafasi kwake kupangwa kikosini.

Laini wakati Bale akiamini hivyo, kuna baadhi ya wachezaji wanaotajwa katika orodha ya kumwangusha Benitez kwa sababu hawakuwa wanaiva.

Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na straika mairi wa kikosi cha Madrid, Cristiano Ronaldo na mlinzi kisiki Sergio Ramos.

Ronaldo na Sergio wamekuwa wakiripotiwa mara kadhaa kulumbana waziwazi na Benitez kiasi cha kuzuka bifu baina yao, lakini kwa upande wa Bale hali hiyo ni tofauti kwani hakuwahi kumpinga kocha huyo.

Benitez amekumbwa na timuatimua hiyo huku akiacha kumbukumbu ya kupoteza mechi tatu kati ya michezo 25 tangu atue Madrid na kipigo kinachohusishwa kuwa ni sababu ya kuondolewa kwake ni mechi dhidi ya Balceona.

Katika mchezo kikosi bora cha Barca kiliitambia Real Madrid kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 mechi ambayo ilipigwa mwezi Novemba, mwaka jana.

Hata hivyo, hatua ya Bale kusikitikia kuondoka inakuja katika mazingira yanayomvumisha winga huyo katika mpango wa kutimkia Manchester United.

Lakini taarifa hizi za kuondoka winga huyo zinakuwa na kinyume na anachoamini mdau mkubwa wa soka la Hispania, Guillem Balague kwamba winga huyo hawezi kuihama Madrid katika kipindi hiki cha mpito.

“Kwanza tujiulize swali la kwanini tuamini kwamba Bale hana furaha,” Balague amenukuliwa na Sky Sports.

“Lakini ninaweza kuwaambia jambo moja, Real Madrid hawana mpango wa kumruhusu Bale aondoke, kinachozungumzwa kwa sasa ni kama tetesi tu,” alisisitiza Balague.

Claudio Ranieri Akiri Kuwa Na Kibarua Kigumu Bila Jamie Vardy
Gazeti La 'Jambo Leo' latua mikononi mwa Kampuni ya Quality Media Group