Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Young Africans, Hassan Bumbuli, amesema tayari uongozi wa klabu hiyo umekutana na beki na nahodha wa kikosi chao Lamine Moro, ambaye alikua anakabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu.

Bumbuli amesema Uongozi umemsikiliza beki huyo na umejiridhisha baadhi ya madai aliyoyato, kuhusu mgongano uliojitokeza dhidi ya Kocha Nasrideen Nabi walipokua mkoani Mtwara kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC mapema mwezi huu.

 “Tulikaa na Lamine wiki iliyopita tukamsikiliza, kwa kuwa jambo lake alilileta kwetu basi tumelitatua na kumpa majibu yeye na kocha kama mkuu wa ufundi,” amesema Bumbuli.

Bumbuli amesema, licha ya kumaliza tofauti hizo bado nyota huyo hakuwa kwenye mipango ya kocha wao katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga.

Amesema kila kitu kitakaa sawa mara baada ya timu kurejea kutoka mkoani Shinyanga, ambapo walikwenda kucheza mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya MWadui FC waliokubali kufungwa 1-0.

Licha ya Nabi kudai kamfukuza kambini kutokana na utovu wa nidhamu, nyota huyo raia wa Ghana alikana na kusema kuwa yeye sio mtovu wa nidhamu, kocha aliona kama anamdharau.

Hoja darasa la saba kukosa ajira serikalini yaibuliwa bungeni
Biden ataka chanzo cha corona kuchunguzwa upya