Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-1 ambao Liverpool iliupata jana dhidi ya West Ham na kuendeleza mwanzo wake mzuri wa upachikaji wa mabao tangu alipojiunga na klabu hiyo.

Salah aliifungia Liverpool bao la kuongoza dakika ya 21 kipindi cha kwanza kabla ya Joel Matip kuongeza bao la pili dakika ya 24, Liverpool walitawala mchezo huo na kipindi cha pili Alex Oxlade-Chamberlain akaifungia Livepool bao la pili dakika ya 55.

Manuel Lanzini aliifungia West Ham bao la kufutia machozi huku Mohamed Salah akirejea na kufunga bao la nne na kuifanya Liverpool kuibika na ushindi wa mabao 4-1.

Liverpool hawakukosea kumrejesha Salah katika ligi kuu ya Uingereza kwani mpaka sasa amefunga jumla ya mbao 10 katika michezo 16 kwenye mashindano yote aliyoichezea Liverpool msimu huu tangu alipotua Anfield akitokea As Roma.

 

Brendan Rodgers aweka rekodi mpya Celtic
Deontay Wilder atangaza vita na Anhtony Joshua