Bingwa wa dunia wa uzito wa juu mwenye mkanda wa WBC, mmarekani Deontay Wilder usiku wa kuamkia leo amshinda pamabno lake dhidi ya Bermane Stiverne kwa KO.

Deontay Wilder hajawahi kupoteza pambano na hili ni pambano la 39 la uzito wa juu kwa Deontay Wilder kushinda na katika mapambano hayo Wilder ameshinda mapambano 38 kwa KO (Knock Out).

Wilder hakupata shida kumtwanga mpinzani wake kwani mapema tu katika raundi ya kwanza Wilder alionyesha umahili wake kwenye masumbwi kwa kumchapa Stiverne kwa KO na kuibuka mshindi kwenye pambano hilo lililopigwa katika ukumbi wa Barclays Center, Brooklyn.

Baada ya ushindi huo Wilder ameendelea kueleza namna anavyotamanai kupigana na bingwa mwingine wa dunia Anthony Joshua.

 

Liverpool wamelamba dume kwa Salah
Video: Ikulu yamfunda Rais Magufuli, usiombe yakukute