Nchini Kenya wanachama wa umoja wa wahadhiri vyuo vikuu (Uasu), Umoja wa wafanyakazi wa vyuo vikuu Kenya (Kusu), Kudheiha na Umoja wa Wataalamu wa Afya na madaktari wa meno (KMPDU) wameapa kutorejea kazini mpaka pale serikali itakapokubaliana kuonyesha pendekezo lake kujibu pendekezo lao la muundo wa mishahara walilolitoa 2017-2021.

Kwa mujibu wa gazeti la The Nation waandamanaji hao wanataka muajiri wao aheshimu na kutekeleza pendekezo lao kama lilivyotolewa.

Katibu mkuu wa Uasu Constantine Wasonga amesema walikuwa hawajapinga agizo la Waziri wa Fedha Ukur Yattani la kutoa fursa ya kuwepo mazungumzo kufikia suluhu.

“Sisi hatujawahi kukataa kukutana na msuluhishi, badala yake anatakiwa kuyafahamisha mabaraza ya vyuo na serikali kupeleka mapendekezo yao, lakini sisi mgomo wetu unaanza rasmi leo ,” aliwaambia waandishi wa habari.

Kufuatia mgomo huo nchini Kenya, Masomo katika vyuo vikuu vya serikali na vyuo vya udaktari yalisimama kuanzia siku ya jana, Alhamisi baada ya wahadhiri na wafanyakazi wa vyuo hivyo na madaktari bingwa kugoma wakidai marekebisho ya muundo wa mishahara.

Ney wa Mitego: Najiona nikienda kuacha kazi ya muziki.
Stamina: Basata na Wizara mnakuza au mnauwa sanaa?