Aliyewahi kuwa beki wa kushoto wa klabu za Simba na yanga Amir Maftah ameonyesha hisia za kuchukizwa na kitendo kilichoonyeshwa na beki na nahodha wa klabu ya Mbeya City Juma Nyosso dhidi ya nahodha na mshambuliaji wa Azam FC John Bocco.

Maftah ambaye pia aliitumikia timu ya taifa, Taifa Stars, ameonyesha hisia za kuumizwa kitendo hicho kwa kuandika ujumbe mzito kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kwa kukumbushia kitendo kama hichoa mbacho aliwahi kufanyiwa na Juma Nyosso wakati akicheza Simba.

Maftah ameandika kwa uchungu na alienda mbali zaidi kwa kumshangaa Nyosso huku akihoji maswali bila kupata majibu yake.

Amir Maftah

Dunian tumeletwa kwa sababu.tukio lililo tokea limenikumbusha machungu ndani ya nafsi yangu…Juma Nyosso si tukio la kwanza kufanya Ushenzi huo….mechi hii yakwenye picha alinifanyia tukio km hilo na kusababisha mm kumpiga kichwa na kutolewa na kadi nyekundu…..najiuliza ila sipati jibu Nyoso ni mtu wa aina gani?dini gani?tamaduni yake ya wapi?….sijapata jibu….

Tayari uongozi wa Azam FC umeshatoa tamko la kulaani kitendo kilichofanywa na Juma Nyosso katika mchezo wa jana dhidi ya John Bocco, na wameliacha suala hilo mikononi mwa TFF kupitia kamati zake ili kufuatilia na kutoa adhabu kwa mchezaji huyo.

Nyosso aliwahi kufanya kitendo kama hicho msimu uliopita dhidi ya Elias Maguli wakati akiichezea Simba na shirikisho la soka lilimuadhibu kwa kumfungia michezo minane.

Wengine wanadai aliwahi kufanya hivyo dhidi ya aliyekua mshambuliaji wa Simba Joseph Kaniki wakati akiitumikia Ashanti Utd, katika michuano ya ligi ndogo mkoani Morogoro mwaka 2007.

Arsene Wenger Ampotezea Jose Mourinho
Kocha Wa Dar es salaam Young Africans Apata Msiba