Mgombea urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli ameendelea kutangaza neema kwa watanzania ambapo jana ilikuwa zamu ya wakazi wa Bagamoyo, Dar es Salaam.

Dk. Magufuli aliwaeleza wananchi wa eneo hilo kuwa kutokana na neema ya gesi iliyoko eneo hilo, serikali yake itahakikisha ujenzi wa bandari ya kisasa itakayokuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo hivyo kuifanya Bagamoyo kuwa falme za kisasa.

“Bagamoyo itajengwa bandari kubwa ambapo meli kutoka Ulaya zitakuwa zinafika hapa. Ukishakuwa na bandari kubwa, viwanda vingi, Bagamoyo patakuwa mahali pa falme za kisasa. Na ndio maana Bagamoyo itakuwa centre ya uchumi wa Tanzania,” alisema

Kadhalika, Dk. Magufuli aliwahakikishia wakazi wa Bagamoyo kuwa serikali yake itawalipa fidia kwa wakati wale wote ambao maeneo yao yatachukuliwa kwa ajili ya uendelezaji wa miradi ya umma.

Aliwaahidi pia wale ambao maeneo yao yalichukuliwa kupisha uwekezaji wa miradi mbalimbali huku malipo yao yakicheleweshwa, atakapoingia madarakani atahakikisha wanalipwa haraka.

“Ukitaka kuendeleza mahali popote ambapo umewakuta wananchi wanaostahili, kwa mujibu wa sheria ni lazima walipwe fidia. Nataka niwahakikishie ndugu zangu wa Nzinga kuwa suala lao tunalijua na hilo ndilo litakalokuwa suala la kwanza la mimi kulibeba na kulishughulikia ili waeze kulipwa fidia,” alifafanua.

 

 

 

 

 

Lowassa Awamulika ‘Mama Na Mtoto’, amjibu Magufuli
Msemo wa ‘Hapa Kazi Tu’ Wamgharimu MC wa Bongo Star Search