Dk John Magufuli, mgombea urais kupitia CCM, ametangaza habari njema kwa wafanyakazi akiahidi kushusha kiwango cha makato ya kodi pamoja kuwaongezea mishahara ili kuboresha maisha yao.

Magufuli ametoa ahadi hiyo jana katika mfululizo wa kampeni zake wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, zilizohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi wanaotarajia kupata maisha bora kupitia uongozi wa mgombe huyo.

Alieleza kuwa anatambua hali ngumu ya maisha waliyonayo wafanyakazi huwavunja moyo wa katika utendaji wa kazi zao hivyo kupunguza uzalishaji nchini.

“Nataka watu wakae maofisini wafanye kazi ya kuwatumikia watanzania badala ya kwenda kuangalia miradi yao kutokana na hali ngumu ya maisha,” alisema.

Dk Magufuli awalenga wafanyakazi wa majeshi mbalimbali pamoja na waalimu na kuwaahidi kuboresha mazingira yao ya kazi na mishahara yao ili waweze kuishi maisha bora na kuendana na wafanyakazi wa kada nyingine nchini.

Katika hatua nyingine, mgombea huyo aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa atafuta ushuru usio wa lazima kwa wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo mama ntilie pamoja na ushuru kwenye vifaa vya ujenzi ili watanzania waweze kumiki nyumba kwa urahisi.

Muigizaji Wa ‘The Vampire Diaries’ Apata Neema
Tanzia: Mgombea Ubunge Afariki